Jumatano , 26th Aug , 2015

Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC kesho usiku watamenyana na wageni wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Mwadui FC ya Shinyanga katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo itaanza Saa 1:00 usiku na Mwadui FC inatarajiwa kuwa kipimo kizuri kwao baada ya juzi kutoka sare ya 0-0 na Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika taarifa yake, Kocha Mkuu wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amesema katika mchezo huo atapata fursa ya kuwajaribu wachezaji wake ambao hawana nafasi kikosi cha kwanza kutokana na wachezaji wake kadhaa kwenda kuchezea timu zao za taifa.