Jumamosi , 24th Oct , 2020

Kikosi cha wachezaji 22 cha Azam FC kimeondoka Dar mchana wa leo kuelekea Morogoro ajili ya mchezo wa raundi ya 8 dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezw Oktoba 26 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri.

Nyota wa Azam Never Tegere (Wa kwanza kushoto), Obrey Chirwa( wa pili kutoka kushoto), Iddi Seleman Nado(Wa pili kutoka kulia) na nahodha Aggrey Moris( wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja.

Taarifa ya kuondoka kwa kikosi hicho imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Azam Fc, Zacharia Thabiti ambapo amesema wanaelekea Morogoro wakiwa na dhamira moja kubwa ya kukusanya alama tatu muhimu.

Azam ni timu pekee ambayo imeshinda mechi zote tangu kuanza kwa VPL ikiwa na alama 21, ikifuatiwa na Yanga yenye alama 16 huku Simba ikikamata nafasi ya tatu ikiwa na alama 13.

Kikosi kamili cha Azam kilichoelekea mkoani Morogoro ni walinda mlango Bennedict Haule na David Mapigano.

Mabeki ni Nicholas Wadada, Abdul Hamahama, Bruce Kangwa, Yakubu Mohamed na Agrey Moris ambaye ndiye nahodha.

Viongo ni Mudathir Yahya, Richard Djodi, Andrew Simchimba, Never Tigere, Frank Domayo, Abdallah Sebo, Ally Niyonzima, Iddy Nado, Daniel Amoah, na Salum Aboubakar.

Washambuliaji waliosafiri na kikosi ni Ayoub Lyanga, Emmanuel Charles, Prince Dube, Obrey Chirwa na Alan Thierry Akono Akono.