Ijumaa , 16th Nov , 2018

Klabu ya soka ya Azam FC imebainisha kuwa kabla ya kuondoka kwenda kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uganda mchezaji wake Nicholas Wadada, walimpa majukumu ya kuhakikisha anaitetea Taifa Stars kwa kutoruhusu kufungwa na Cape Verde.

Nicholaus Wadada siku aliyotambulishwa Azam FC.

Msemaji wa Azam FC Jaffar Idd ameweka wazi hilo kwa kusema wadada ambaye anacheza nafasi ya mlinzi wa pembani wamempa majukumu kama timu akahakikishe anajituma ili wapate matokeo mazuri ambayo pia yatailinda Taifa Stars.

''Tafadzwa Kutinyu ameondoka jana kwenda kujiunga na Zimbabwe lakini Nicholaus Wadada aliondoka muda na kwa kuzingatia kuwa mchezo wa Uganda unatuhusu pia tulimwambia akahakikishe anapambana kwelikweli ili nasi tupate nafasi'', amesema.

Nicholaus Wadada aliyezungushiwa duara akiwa na kikosi kilichoshinda 3-0 dhidi ya Lesotho.

Tanzania ina nafasi ya kufuzu AFCON 2019 endapo itaifunga Lesotho huku Uganda nayo ikiifunga Cape Verde ugenini hivyo Taifa Stars itafikisha alama 8 ikibakiwa na mezhi 1 wakati Cape Verde watabaki na alama zao 4 na mechi moja hivyo watakuwa wameaga rasmi.

Uganda na Cape Verde wanachezaji kesho Jumamosi Novemba 17 huku Taifa Stars ikicheza Novemba 18 siku ya Jumapili.