Kikosi cha Azam
Bao la Azam katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo wake 'Chumvi' Frank Domayo katika dakika ya 33 ya mchezo kufutia ubunifu binafsi wa kukimbiza mpira na kumchambua golikipa wa Taifa kwa shuti kali.
Pia katika hatua nyingine jopo la makocha limemchagua kiungo wa Azam FC na mfungaji wa bao Frank Domayo kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo ambapo amezawadiwa kitita cha shilingi milioni 1.
Azam sasa itakutana Simba katika mchezo wa fainali utakaopigwa Ijumaa, tarehe 13, Januari
Wakati Azam ikitinga fainali, uongozi wa klabu hiyo leo jijini Dar es Salaam imemtambulisha kocha wake mpya ambaye ni Aristica Cioaba kutoka nchini Romania akiwa na uzoefu wa kufundisha vilabu kadhaa katika bara la Afrika.