Jumatatu , 11th Oct , 2021

Timu ya taifa ya Soka Ufaransa imeweka ekodi ya kibabe baada ya kubeba ubingwa wa michuano ya Ligi ya mataifa barani Ulaya yaani ‘UEFA Nations League’ baada ya kuifunga Uhispania mabao 2-1 usiku wa kuamkia leo.

Timu ya Ufaransa ikisheherekea ubingwa wa UEFA Nations League baada ya kuwafungwa Uhispania 2-1 usiku wa kuamkia leo Oktoba 11, 2021.

Hispania ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake Mayol Oryazbal dk66' lakini baadae Ufaransa wakasawazisha kupitia ka mshambuliaji wake Hatari, Karim Benzema dk68' kabla ya Kylian Mbappe kuuotea mtengo wa kutoa wa walinzi wa Uhispania na kufunga bao la ushindi dk80'.

Rekodi waliyoiweka Ufaransa ni kuwa timu ya taifa ya kwanza kwenye historia kuwahi kubeba Ubingwa wa kombe la Mataifa ya Ulaya ‘UEFA EUROS’ ya mwaka 2000, Kombe la Dunia 1998 na mwaka 2018 pamoja na Ubingwa wa UNL.

Mafanikio hayo yanaonekana kutuliza hali ya hewa juu ya hatma ya kibarua cha Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps ambaye hakuwa na mwendo mzuri kwenye michezo yake mitano iliyopita kwa kushindwa kupata ushindi.

Didier Deschamps pia ameweka rekodi ya kuwa kocha pekee aliyebeba Ubingwa wa kombe la Dunia 2018 akiwa na Ufaransa na kubeba tena ubingwa UNL akiwa pia na Ufaransa.

Mbali na sherehe hizo za Ubingwa, wasimamizi wa michuano hiyo, Shirikisho la Soka barani Ulaya, ‘UEFA’ limemtangaza kiungo wa Uhispania Sergio Busquetskuwa mchezaji bora wa mashindano na Kylian Mbappe, mfungaji bora.

Mbappe amekuwamfungaji bora baada ya kufunga mabao 2 na kuwapiku mchezaji mwenzake wa Ufaransa Karim Benzema na Ferran Torres wa Uhispania waliokuwa na mabo mawili ila yeye akijitofautisha kwa kutoa Assist 2.