Jumatatu , 9th Nov , 2020

Kiungo wa Bayern Munich, Joshua Kimmich atakaa nje ya uwanja hadi mwezi Januari baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti aliloumia Jumamosi iliyopita wakati The Bavarians ilipoitandika Borussia Dortmund bao 3-2.

Kiungo wa Bayern Munich, Joshua Kimmich (wapili kutoka kulia)akitolewa uwanjani baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Borussia Dortmund

Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 25, aliondolewa dimbani dakika ya 36 baada ya kujaribu kumzuia Erling Haaland na kwa bahati mbaya alijikuta akipata jeraha.

Taarifa rasmi kutoka klabuni hapo zimeongeza kwamba upasuaji wa goti la Kimmich umefanyika kwa mafanikio na atakosa mechi za timu yake ya Taifa dhidi ya Ukraine, Hispania na Jamhuri ya Czech.

Kimmich amekuwa msaada mkubwa kwa Bayern tangu kuondoka kwa Thiago Alvantara aliyetimkia katika klabu ya Liverpool nchini Uingereza .