Alhamisi , 22nd Apr , 2021

Karim Benzema amefunga magoli mawili katika mchezo wa jana dhidi ya Cadiz ambapo Real Madrid aliibuka na ushindi wa 3-0.

Ushindi huo unawafanya Real Madrid kuongoza ligi wakiwa na alama 70 wakifuatiwa na Atletico Madrid wenye alama hizo lakini wananufaika na matokeo yao wenyewe walipokutana'head to head'kufuatia kanuni wanayoitumia katika ligi hiyo.

Ladha ipo katika mbio za kufukuzia tuzo ya mfungaji bora wa msimu kwa la liga maarufu kama 'Pichichi' ambapo Karim Benzema amefikisha magoli 21 akiwa sawa na nyota wa Barcelona Lionel Messi ambao wote wana magoli 21.

Wadau wengi hawakufikiri endapo Benzema anaweza kushindana na Messi kwa kiwango hiki hasa baada ya Ronaldo kuondoka Madrid na kwenda kujiunga Juventus ,wakiamini ufalme utabaki upande moja tu.

Msimu uliopita Bemzema alifunga goli 21 na kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa licha ya kutokuwa mfungaji bora wa jumla, ambapo Lionel Messi aliyeibuka kinara wa ufungaji kwa magoli yake 25 .

Msimu huu ambao umebakiza mechi 6 kwa Real Madrid na 8 kwa Barcelona mbio za ufungaji bora bado zipo kwa mafahari hawa wawili Benzema na Messi ambao kila moja anagoli hizo 21 .

Orodha ya wafungaji wanaoongoza kwa magoli hadi sasa,haitofautiani ile iliyomaliza msimu uliopita kwenye nafasi 4 za juu unaweza kusema jamaa wamelinda viwango vyao.

Lionel Messi 21 (Barcelona)

Karim Benzema 21(Real Madrid)

Gerrard Moreno 18 (Villareal)

luis Suarez 16 (Atletico Madrid)

ITALIA

Inter Milan ilitoka sare ya bao moja dhidi ya Pezia na kushindwa kuongeza wigo wa alama walizonazo kileleni ingawa wana nafasi nzuri ya kutwaa kombe la ligi kuu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10.

Bao la Spezia lilifungwa na Diego Farias dakika ya 5 wakati la Inter lilifungwa na Ivan Perisic dakika ya 39 na sasa wanafikisha alama 76 wakiwa wamecheza michezo 32.

Juventus iliibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Parma, mabao yao yakifungwa na Alex Sandro aliyefunga mara mbili na Matthijs De ligt huku la kufutia machozi la Parma likifungwa na Gaston Brugman.

Juventus imesogea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 65 katika michezo 32.

Ac Milan walijikuta wakipoteza dhidi ya Sassoulo kwa bao 2-1 licha ya kwamba wanaendelea kushikilia nafasi ya pili wakiwa na alama 66.

UINGEREZA

Manchester City iliibuka na ushindi wa bao 2-1, mabao ya Phil Foden na Rodri huku la utangulizi la Villa lilifungwa na John MacGinn.

City imefikisha alama 77 katika michezo 33,wakiiacha Man United kwa alama 11 ingawa The Red Devils wana michezo miwili hawajacheza.

Tottenham Hotspurs ilipata ushindi wake wa kwanza chini ya Kocha wake wa muda, Ryan Mason walipoinyuka Southampton bao 2-1.

Heung Min Son na Gareth Bale walifunga mabao hayo yaliyowasaidia kufikisha alama 53 na kukwea hadi nafasi ya 6 katika msimamo wa EPL.

UJERUMANI

Erling Haaland alifunga bao katika ushindi wa Borussia Dortmund wa bao 2-0 dhidi ya Union Berlin na sasa wameimarika katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Bundesilga wakiwa na alama 52.

Hoffeinheim ilishinda bao 3-2 dhidi ya Borussia Monchegladbach ,VFB Stuttgart ilinyukwa bao 3-1 na VFL Wolfsburg,Werder Bremen ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Mainz.