Jumanne , 15th Feb , 2022

Hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa Barani Ulaya inataraji kuanza kuchezwa usiku wa leo Februari 15, 2022 kwa michezo miwili ambapo Real Madrid itacheza ugenini dhidi ya PSG huku Sporting Lisbon itakuwa wenyeji wa Manchester City michezo yote saa 5:00 usiku.

(Karim Benzema wa Madrid na Sergo Ramos wa PSG kwenye picha ndogo)

 

Madrid wamemjumuisha mshambuliaji wake tegemezi Karim Benzema kikoisni huku, PSG wakisema Neymar atarejea ilhali Sergio Ramos atakosekana na Lionel Messi kucheza na Madrid kwa mara ya kwanza bila ya kuwa mchezaji wa Barcelona.

Kukosekana kwa Ramos kutokana na maumivu ya misuli na kunamfanya gwiji huyo wa Real Madrid kukosa nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani aliyoichezea kwa mafanikio makubwa kwa miaka 16. Kwenye michezo 10 waliyokutana wawili hai, Madrid ameibuka mshindi mara 4, sare 3 na PSG kupata ushindi michezo 3.

Kwa Upande wa Manchester City, watashuka dimbani wakiwa na hatihati ya kuwakosa nyota wake Jack Grealish, Gabriel Jesus wenye maumivu na Kyle Walker anayetumikia adhabu ya kuoneshwa kadi nyekundu. Rekodi zinaonesha City ameshinda mara 1, kufungwa 2 na Sporting lisbon kwenye michezo 3 waliyocheza.