
Uwanja wa Amaan Zanzibar
Taarifa za mapema hii leo zilieleza kuwa Shirikisho la soka barani Afrika ( CAF) limeliagiza shirikisho la soka nchini Tanzania ( TFF) kuhamishia maandalizi ya mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho mnamo 25/5/2025 baina ya Simba dhidi ya Berkane kupigwa kwenye dimba la Amaan visiwani Zanzibar.
Berkane wameeleza kuwa "Uwanja wa Amaan Zanzibar utapigwa mchezo wa marudiano Kombe la shirikisho la Afrika "
Wakati huo huo Simba kupitia mitandao ya kijamii wamesema kuwa "Taarifa rasmi kuhusu uwanja wa mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itatolewa baada ya mchezo wa awali utakaochezwa Jumamosi Mei 17, 2025."