Biashara united wakiminyana na Azam FC uwanja wa CCM Kirumba
Mabo ya ushindi ya Biashara kwenye mchezo huu yamefungwa na Collins Opare aliyefunga bao la kwanza dakika ya 49 na James Shangara alifunga bao dakika ya 90. Huu ni ushindi wa kwanza kwa Biashara baada ya kucheza michezo 10 bila ushindi ambapo kabla ya mchezo wa leo walikuwa wametoka sare michezo 7 na walifungwa michezo 3 kwenye michezo 10 ya mwisho.
Ni kwa mara ya kwanza Biashara wanaifunga Azam FC katika michezo 7 ya Ligi Kuu kabla ya leo walikuwa wamefungwa mara 2 na sare 2. Kwa ushindi huu Biashara wanapanda kutoka nafasi ya 14 hadi 12 wamefikisha alama 15 katika michezo 15, wakati Azam FC wamesalia nafasi ya 3 na alama zao 24.
Ligi itaendelea tena kesho kwa mchezo mmoja Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Yanga SC, mchezo huu utachezwa uwanja wa Manungu Complex na utachezwa Saa 10: 00 Jioni.

