Jumanne , 26th Oct , 2021

Klabu ya Biashara United Mara imetolea majibu taarifa zinazoenea mitandaoni kuwa, Viongozi wa klabu hiyo walipokea rushwa ili kukwamisha safari ya timu hiyo kwenda nchini Libya mapena wiki iliyopita ili kucheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Al Ahly Tripoli.

(Kikosi cha Klabu ya Biashara United Mara msimu wa mwaka 2021-22.)

Biashara United baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya makamu hao bingwa wa Libya ilitakiwa kusafiri kwenda Libya kucheza mchezo wao wa marudiano Oktoba 23, 2021 lakini ilishindwa kufanya hivyo kwa kile walichodai kuwa walikosa vibali vya kurusha ndege yao yakukodi.

Barua ya Klabu hiyo imeeleza kuwa:

(Barua ya klabu ya Biashara United Mara)

Biashara United kwasasa inasubiri taarifa rasmi kutoka Shirikisho la Soka Afrika CAF kujua hatma ya mchezo huo kama upo au wameshaondolewa kwenye michezo hiyo ya kuwania kufuzu makundi ya kombe la Shirikisho Afrika.