Jumapili , 25th Oct , 2020

Fainali ya ligi ya taifa ya mpira wa kikapu Tanzania inatarajiwa kupigwa leo kwa michezo kwa upande wanaume na wanawake .

Mshikemshike wa mpira wa kikapu Tanzania.

Kwa upande wa wanaume timu ya Kurasini Heat watakua wakipepetana na Oilers mchezo utakaopigwa saa 10 jioni katika uwanja wa Don Bosco Upanga.

Kurasini Heat wametinga hatua hiyo baada ya kuwanyuka Panthers kwa alama 72-55 katika hatua ya robo fainali wakati Oilers wao walitinga fainali kwa kuwanyuka Vijana City Bulls kwa alama 78-72

Kwa matokeo hayo Vijana watacheza dhidi ya Panthers katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa mashindano hayo ya taifa upande wa wanaume itakayochezwa majira ya saa sita mchana

Katika kusaka bingwa kwa upande wa wanawake JKT Stars itaumana na Don Bosco Lioness saa nane mchana nao vijana Queens wanacheza na Jeshi Stars.

Bingwa kwa upande wanaume ataiwakilisha nchi katika mashindano ya ligi ya vilabu bingwa Afrika huku mshindi wa pili na watatu watacheza michuano ya kanda ya tano.

Vilevile bingwa kwa upande wa wanawake ataiwakilisha nchi katika michuano ya Afrika na kanda ya tano.