Jumatatu , 12th Jun , 2017

Mwanariadha maarufu duniani kutoka Jamaica, Usain Bolt amewaaga rasmi mashabiki wake kushiriki mashindano ya riadha nchini humo kwa kushinda mbio za mita 100.

Usain Bolt

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mshindi wa medali 8 za dhahabu katika michuano ya Olimpiki, ameshinda kwa urahisi katika mashindano ya mita 100 yaliyofanyika juzi huko Kingstone, Jamaica kwa kutumia sekunde 10.03.

Mbali na ushindi huo aliyoupata, Bolt alikiri kuwa haikuwa kazi rahisi kwa kuwa alijawa na uoga kwa kuogopa kuaga mashabiki wake kwa aibu.

“Nimezoea kuona mashindano yote kama ya kawaida tuu kwani huwa najiamini sana,  ila ya leo nimeona migumu sana na nilishikwa na hofu kama ningeshindwa ningeumia sana kuwaaga mashabiki wangu “alisema Usain Bolt kwenye mahojiano wakati wa mahojiano.

Mwanariadha Usain Bolt

Hata hivyo Usain Bolt anatarajia kustaafu mchezo huo mwezi Agosti mwaka huu baada ya mashindano ya dunia ya riadha yatakayofanyika London, Uingereza.