Jumanne , 3rd Jun , 2025

Kiungo mshambuliaji wa Manchester United Bruno Fernandes amekataa ofa nono kutoka katika klabu ya Al Hilal inayoshiriki ligi kuu ya Saudi Arabia (Saudi Pro League).

Bruno mwenye umri wa miaka 30 mpaka hivi sasa ndiye mchezaji aliyehusika katika upatikanaji wa magoli mengi zaidi akihusika kwenye magoli 18 ndani ya kikosi cha Manchester United msimu huu, amefunga magoli 8 na kutoa assist 10.

Licha ya kuwekewa dau kubwa mezani lakini taarifa kutoka barani Ulaya zinasema kuwa Mreno huyo amechukua uamuzi wa kuendelea kucheza soka barani Ulaya kwa kuamini kuwa ndiko kwenye soka bora zaidi.