Jumanne , 3rd Jun , 2025

Chelsea imethibitisha kuwa haitampa mkataba wa kudumu  Muingereza Jadon Sancho  badala yake watalipa faini ya pauni milioni 5 ambayo ni sawa na shilingi  bilioni 18,154,985,000 kwa fedha za Tanzania  ili kumrudisha mchezaji huyo katika klabu yake ya  Manchester United.

Jadon Sancho

Winga huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na United 2021 akitokea Borussia Dortmundkwa ada ya  pauni milioni 73 huku akijiunga na  Chelsea kwa mkopo msimu uliopita baada ya kutokuwa na uhusiano mzuri dhidi ya Erik ten Hag aliyekuwa kocha mkuu wa Manchester United.

Chelsea wanalazimika kulipa faini hiyo baada ya kukubali kumnunua Sancho kwa ada ya takribani pauni milioni 25 ikiwa wangemaliza kwenye nafasi 6 za juu za EPL lakini baadae wakabadili mpango huo.