(Juventus na Mabingwa watetezi wa UEFA Chelsea 'The Blues')
Kuelekea kwenye mchezo huo, Bingwa mtetezi Chelsea huenda akawakosa wachezaji wake kadhaa Ben Chilwell, Callum Hodson Hodoi na Recce James wenye majeraha huku Mason Mount akifanya mazoezi ya pamoja na kikosi.
Chelsea itacheza na Lille kwenye dimba la Stamford Bridge nchini England kwenye mchezo huo ambapo mara ya mwisho wawili hao kukutana ilikuwa mwaka 2019 ambapo Chelsea iliifunga Lille mabao 2-1 nyumbani na Ugenini.
Kwa upande mwingine, Wababe wa Italia, klabu ya Juventus itashuka dimbani kucheza ugenini dhidi ya nyambizi wa Hispania klabu ya Villarreal ikiwa ni kwa mara ya kwanza wawili hao kukutana tangu mwaka 2009 ambapo Villareal ilishinda 4-1.
Juventus ipo huenda ikacheza bila nyota wake kadhaa ambao wana maumivu kiasi licha ya kuendelea na mazoezi mepesi kama vile Federico Bernardeschi, Federicco Chiesa, Paul Dybala na Geogio Chiellini.
Michezo ya hatua ya 16 bora inataraji kuendelea tena Jumatano ya kesho Februari 22, 2022 ambapo watukutu wa Diego Simeone Atletico Madrid watawakaribisha Manchester United ilhali Benifica watacheza na Ajax.


