(Kai Havertz akifunga bao dhidi ya Lille ya Ufaransa)
Mabao ya Chelsea yamefungwa na washambuliaji wake Kai Havertz na Christian Pulisic na kubeba matumaini makubwa ya kufuzu hatua ya Robo fainali ya michuano hiyo kuelekea Machi 16, 2022 kwenye mchezo wa marudiano.
Ushindi huo umeifanya Chelsea kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka nchini England kushinda michezo mitano mfululizo bila kuruhusu bao kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya na Duniani.
Chelsea pia imecheza michezo 16 mfululizo ya michuano yote bila kupoteza kwenye dimba lake la Nyumbani ‘Stamford Bridge’ ikishinda michezo 11 na kutoa sare michezo 5 pekee.
Kwa Upande wa Juventus, wametoka sare ya 1-1 dhidi ya Nyambizi wa Uhispania, Villarreal na bao lake limefungwa na Dusan Vlahovic dakika ya 1 na kuwek arekodi kuifungia Juventus mapema zaidi na kuliko Alessandro Del Piero.
Dani Parejo aliwasawazishia Villarreal dakika 66 na kutibua uongozi wa Juventus na kuifanya Juventus kuweka rekodi mbaya ya kushindwa kupata ushindi kwenye michezo ya mkondo wa kwanza katika misimu minne mfululizo.



