
kikosi cha Yanga
Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Agosti 16, ulishuhudia mashabiki wake wakifanya fujo hizo wakati kikosi hicho kiliposhinda mabao 2-1.
Hatua hiyo inajiri baada ya Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB) kukaa kikao chake cha Agosti 26 kwa ajili ya kupitia mwendendo wa matukio mbalimbali.
Kosa hilo linatokana na mashabiki hao kurusha chupa hizo uwanjani hapo wakati mchezo huo ukiendelea.
Taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo ilieleza adhabu hiyo ni kwa mujibu wa uzingativu wa kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu Bara kuhusu udhibiti kwa klabu.
Mbali na adhabu hiyo Yanga pia imetozwa faini ya sh 500, 000 kwa kosa la kufanya mabadiliko ya wachezaji kwa mikupuo minne badala ya mitatu kama ilivyoanishwa kwenye kanuni ya 17:32 ya Ligi Kuu Bara kuhusu taratibu za mchezo.
Mabadiliko hayo yalifanyika wakati wa mchezo wa klabu hiyo dhidi ya Coastal Union walioibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Agosti 20, adhabu hiyo ni kwa uzingativu wa kanuni ya 17:60 ya ligi kuu kuhusu taratibu za mchezo.
katika hatua nyingine Mwamuzi wa akiba kwenye mchezo huo, Abel William kutoka Arusha na msaidizi namba moja, Ferdinand Chacha kutoka Mwanza wamepewa onyo kali kwa kushindwa kusimamia na kutuza kumbukumbu za mabadiliko ya wachezaji hao.
Adhabu hii ni kwa uzingativu wa kanuni ya 42:1(1.6) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa waamuzi.