Jumanne , 6th Jul , 2021

Mashindano ya Langalanga ya Australian Grand Prix yaliyopangwa kufanyika Novemba 19-21 mwaka huu yamefutwa kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na janga la Corona.

Picha inaonyesha namna mashindano ya Australian Grand Prix yanavyofanyika.

Mwenyekiti wa ushirikiano wa Australian Grand Prix , Paul Little amesema hawajafurahishwa na taarifa hiyo ingawa wanakubaliana na ukweli juu ya changamoto zinazoikumba Australia juu ya sheria za kimataifa za vikwazo kwenye usafiri pamoja na suala la chanjo.

Mnamo mwaka 2020,Australian Grand Prix iliahirishwa kutoka machi 14 hadi Novemba mwaka huu kutokana na kufungwa wa mipaka ya nchi hiyo.

Kufuatia taarifa hiyo, Malaysia Motor GP,imesogzwa mbele kutokea Oktoba 22 hadi 24 ambayo ndio tarehe iliyopangwa kufanyikwa kwa mashindano ya Australia.