
Nyota wa Golden State Warriros, Stephen Curry.
Curry ameipiku rekodi iliyokuwa inashikiliwa kwa muda mrefu na Guy Rodger aliyekuwa na assisti 4,855 na kufikisha assisti 4,856 na kuwa mchezaji mwenye assisti nyingi wa muda wote kwenye histori a ya timu ya Golden State Warriors mpaka hivi sasa.
Tim Hardaway anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na assisti 3, 926, Rick Barry mwenye assisti 3,247 na Chris Mullin anashika nafasi ya tano akiwa na assisti 3, 146.
Mbali na kuwa kinara wa assisti wa kihistoria kwenye timu hiyo, lakini Curry pia ni kinara wa kishisotia wa kuvuna alama 3 nyingi zaidi kwa kurusha mpira nje ya eneo la D la uwanja wa kikapu na kutinga kwenye kikapu hiko (3-pointers).
Kwa upande mwingine,
Ligi ya kikapu nchini Marekani NBA, inataraji kuendelea tena usiku wa kumakia kesho kwa michezo 7, Vinara wa upande wa Magharibi, Utah Jazz watakuwa ugenini kukipiga na Boston Celtics saa 8:30 usiku ilhali vinara wa Mashariki Philadelphia 76ers watacheza na New york Knicks saa 9:00 usiku.
Bingwa mtetezi wa ligi hiyo, Los Angeles Lakers watajitupa dimbani dhidi ya Minnesota Timberwolves saa 11:30 Alfajiri ya kuamkia kesho.