
Akizungumza na East Africa Radica Radio, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa wavu mkoa wa Dar es salaam, Siraju Mwasha amesema, timu zilizoondoka ni tatu ambapo ni kutoka Ilala, Temeke pamoja na timu kutoka Makongo.
Kwa upande mwingine Mwasha amesema, timu hizo zitakaporudi kutoka Iringa zitaendelea na ligi ya mpira wa wavu mkoa wa Dar es salaam ambapo zimefikia hatua ya Play Off huku timu nne kwa wanawake na nne za wanaume zikiwa zimeingia katika hatua hiyo.
Mwasha amesema, timu zilizoingia katika hatua hiyo kwa upande wa wanaume ni Jeshi Stars, Magereza, Feature na Polisi Marine huku kwa upande wa wanawake kukiwa na timu za JKT, Jeshi Stars, Magereza na Makongo.