
Mlinzi nyota wa Denver Nuggets, Will Barton.
Akiongea kwa uchungu, Malone amesema namna orodha ya wachezaji wake wenye majeraha inavyozidi inampa wakati mugmu ukizingatia mlinzi mwingine tegemezi Jamal Murray amepata majeraha na imethibitika ataikosa michezo yote iliyosalia msimu huu kwenye NBA.
Barton amepata maumivu hayo wakati akiwa kwenye kasi ya kujaribu kumtoka mlinzi wa Golden State Warriros jambo lililopelekea wapoteze mchezo huo kwa kumkosa nyota huyo mwenye wastani wa kupata alama 12.7 kwenye michezo 56 ikiwemo 52 aliyoanza kikosini.
Barton na Murray kwa pamoja wameisaidia Denver Nuggets kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo ya NBA kwa upande wa Magharibi na kuwa na muendelezo wa kupata matokeo mazuri kwani wamefungwa mchezo mmoja kwenye michezo mitano iliyopita.
NBA inataraji kuendelea tena usiku wa kuamkia kesho kwa michezo 11 huku mabingwa watetezi, Los Angeles Laker wakitaraji kukipiga na Orlando Magic, Piladelphia 76ers vinara wa upande wa mashariki watacheza na Oklahoma City Thunder, muda mmoja wa saa 12 alfajiri.