
Katika mchezo huo, goli kipa wa mabingwa hao, Deogratius Munishi 'Dida' ameweza kuisaidia timu yake kwa hali ya juu baada ya kuokoa mikwaju ya penati baada ya dakika 90 za mchezo kukamilika kwa sare ya bila ya kufungana.
Kwa matokeo hayo, Yanga SC itakutana na AFC Leopard ya Kenya katika nusu fainali ya kwanza ya kutafuta tiketi ya kuingia fainali kati yao.