Jumatano , 5th Aug , 2015

Dirisha la Usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Ligi Daraja la kwanza (FDL), na Ligi Daraja la Pili (SDL) linatarajiwa kufungwa kesho saa sita usiku.

Katika taarifa yake, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto amesema, vilabu vyote vinavyoshirki msimu mpya wa 2015/2016 wanavikumbusha kuhakikisha vinakamilisha usajili wa wachezaji wao kabla ya dirisha la usajili kufungwa kesho hapo kesho.

Kipindi cha dirisha la usajili kwa timu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kilifunguliwa Juni 15 mwaka huu ambapo kitamalizika hapo kesho kwa awamu ya kwanza ya usajili.