Jumatatu , 24th Jan , 2022

Droo ya makundi ya michuano ya mataifa Africa (Afcon) kwa mwaka 2023 nchini Cote d’Ivoire inatarajiwa kufanyika mjini Douala nchini Cameroon siku ya Ijumaa January 21,2022 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka barani Africa (CAF).

Kiungo wa Ivory Coast, Frank Kessie akijaribu kuwatambuka mabeki wa timu ya Taifa ya Morocco katika mechi moja wapo za Kirafiki.

Droo hiyo itachezeshwa na nahodha wa zamani wa Cameroon Rigobert Song ambaye ameshiriki kwenye michuano ya Afcon mara 8 huku akitwaa kombe hilo mara 2 (2000 na 2002) huku akisaidiwa na kiungo wa zamani wa Nigeria Emanuel Amunike ambaye alitwaa kombe la Afcon mwaka 1994.

Makala hayo ya 34 itahusisha kwanza hatua ya awali ya mtoano kwa timu 12 ambazo zinashika viwango vya chini kwa ubora wa soka duniani kutokea barani Afrika kwa kucheza nyumbani na ugenini kisha washindi 6 kujumuika na timu 42 kwa ajili ya hatua ya kufuzu kwenye michuano hiyo.

Timu ambazo zitaanza kwenye hatua ya awali zinahusisha

Kundi 1: Lesotho, Eswatini, Botswana, Gambia, South Sudan, Mauritius

Kundi 2: Chad, Sao Tome & Principe, Djibouti, Somalia, Seychelles, Eritrea