
Michuano ya vijana chini ya miaka 17
Upangaji wa droo hiyo utafanyikia kuanzia saa 1:00 usiku katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, ukiratibiwa na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF na Shirikisho la Soka Tanzania TFF ambao ndiyo wenyeji wa michuano hiyo.
Timu zilizofuzu kushiriki michuano hiyo ni pamoja na Mwenyeji, Tanzania, Angola, Cameroon, Guinea, Morocco, Nigeria, Senegal and Uganda.
Fainali za michuano hiyo zinatarajia kufanyika kuanzia April 14 hadi 28, 2019 ambapo timu zitakazofuzu hatua ya nusu fainali, zitaliwakilisha bara la Afrika katika michuano ya Dunia ya vijana chini ya miaka 17 itakayofanyika mwakani nchini Peru.