Jumatano , 21st Aug , 2019

Droo ya hatua ya mtoano ya michuano ya Sprite Bball Kings 2019 imefanyika hii leo katika ofisi za EATV & EA Radio Jijini Dar es Salaam.

Kwenye droo ya Sprite Bball Kings

Michuano hiyo inayoandaliwa na East Africa TV na East Africa Radio kwa kushirikiana na kinywaji cha Sprite, inafanyika kwa msimu wa tatu ambapo jumla ya timu 42 zimepangwa katika hatua ya mtoano itakayofanyika Jumapili, Agosti 25.

Akizungumza katika ufunguzi wa semina ya timu shiriki za michuano hiyo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Michael Mwita ameishukuru EATV na EA Radio pamoja na Sprite kwa kufanikisha mashindano haya kwa masimu wa tatu. 

"Tunapenda kuwashukuru EATV kwa kushirikiana na Sprite, kufanikisha mashindano ya Sprite Bball Kings kwa msimu wa tatu sasa, ni mafanikio makubwa sana", amesema Mwita.

"Kutokana na vijana kuonekana kupitia EATV, tumefanikiwa kuwashawishi mabingwa wa NBA, Toronto Raptors kuja nchini. Hii ni kutokana na video ambazo tuliwatumia", ameongeza.

Ratiba nzima ya hatua ya mtoano ni kama inavyoonekana hapo chini. 

 

Kivumbi cha hatua ya mtoano ya Sprite Bball Kings 2019 kitafanyika katika viwanja vya JMK Park Jijini Dar es Salaam, Jumapili ya Agosti 25 kuanzia saa 2:00 Asubuhi.