Jumatatu , 30th Mei , 2022

Uongozi wa klabu ya Singida Big Stars zamani DTB umeamua kupeleka makazi ya timu hiyo mkoani Singida huku wakitarajia kuutumia uwanja wa Namfua uliopo mkoani humo kama uwanja wao wa nyumbani.

kikosi cha DTB

Wakati klabu hiyo inaitwa DTB, ilikuwa ikiutumia uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam kama uwanja wa nyumbani hivyo baada ya kubadili jina la timu hiyo sasa rasmi itakuwa inatumia uwanja wa Namfua.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurungezi mtendaji wa klabu hiyo, Muhibu Kanu alisema wao kama uongozi wamefanya taratibu zote za kubadili jina la timu hiyo pamoja na kuyaamisha makazi.

"DTB ilikua inamilikiwa na Benki, sasa timu hii wameichukua wengine na hao wameamua kuibadili jina la timu na tayari tumeshakamilisha taratibu zote za kisheria" amesema  Muhibu na kuongeza;