
Baadhi ya mastaa wa DTB ambayo imepanda Ligi Kuu msimu ujao
Historia ya DTB ni kwamba ilianza kama sehemu fulani ya burudani kwa wafanyakazi wa Benki ya Diamond Trust kwa maana kila baada ya muda wa kazi walikusanyika na kufanya mazoezi kwa pamoja huku wakiwa wanacheza michezo mbalimbali na baadhi ya timu zikiwemo za Veterans.
Baada ya msimu mmoja baadae waliamua kuisajili rasmi na kushiriki Ligi ya Wilaya ya Ilala kama ilivyokuwa kwa Azam Fc na kuanza kufanya sajili nzuri na bora huku wakiuwa na malengo ya kupanda kila hatua waliyopitia.
Haikuchukua muda mrefu sana kupata mafanikio yao na yalianza kuonekana kwa kufanikiwa kucheza Daraja la kwanza.
Klabu hiyo ilifanya usajili wa kutisha kwa kunyakua wachezaji walio na uzoefu katika Ligi Kuu Tanzania bara kama ifuatavyo
-Owen Chaima,Tafadzwa Kutinyu,James Kotei,Yusuph Mlipili, Juma Abdul, Hamis Tambwe,Shafiq Batambutze, Johnson Clement,Chunga Elly n.k hayo ni baadhi ya majiba makubwa yaliyopo kwenye kikosi hicho cha DTB kilichopanda Ligi Kuu.