Jumatatu , 27th Jan , 2020

Bingwa mara tano wa ligi ya kikapu nchini Marekani (NBA), Kobe Bryant amefariki katika ajali ya ndege binafsi aliyokuwemo yeye na watu wengine saba kwa mujibu wa ripoti mbalimbali nchini Marekani.

Kobe Bryant na mwanaye 'Ginni'

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia Jumatatu, Januari 27, 2020 kwa saa za Afrika Mashariki wakati nchini Marekani ni majira ya mchana katika eneo la Calabasas, jimbo la California, ambapo helikopta hiyo ilianguka na kuungua huku kukiwa hakuna yeyote aliyenusurika.

Dunia nzima imeshtushwa na kifo cha mkongwe huyo pamoja na mwanaye wa kike Gianna mwenye umri wa miaka 13, miongoni mwao ni Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ambaye aliandika katika mtandao wa Twitter akisema, "Kobe alikuwa ni mtaalamu katika 'court' na alianza katika kitu kingine cha pili. Kumpoteza Gianna ni maumivu makali sisi kama wazazi. Mimi na Michelle tunatuma salamu za rambi rambi na tunawaombea Vanessa na familia nzima ya Bryant kwenye siku hii ambayo haifikiriki".

Naye rasi wa sasa wa Marekani, Donald Trump amezungumzia msiba huo mzito akisema kuwa Bryant licha ya kuwa mchezaji bora wa muda wote wa kikapu, alikuwa ndiyo anaanza katika maisha, aliipenda familia yake na kitendo cha kumpoteza mtoto wake Gianna ndiyo maumivu makali zaidi.

Baadhi ya rekodi zake ndani ya NBA ni:
 

Bryant ambaye mwaka 2018 alishinda tuzo ya Academy kupitia filamu yake fupi ya  “Dear Basketball", alikuwa na mke mmoja aitwaye Vanessa na watoto wanne ambao ni Gianna, Natalia, Bianca na Capri na baada ya Kobe Bryant kufariki akiwa na binti yake wa pili kuzaliwa aitwaye Gianna mwenye miaka 13 ambaye pia alikuwa anacheza Kikapu, sasa ameacha mke na watoto watatu.