Jumanne , 20th Mei , 2025

Kocha  wa Chelsea Enzo Maresca amesema hafurahishwi na kitendo cha wapinzani wao Real Betis kupewa siku mbili za ziada kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa fainali wa Uefa Conference League utakaopigwa Mei 28 2025

Enzo Maresca - Kocha  wa Chelsea

Laliga wamekubali ombi la Real Betis la kuurudisha nyuma mchezo wao dhidi ya Valencia ambao hapo awali ulipangwa kuchezwa Jumapili ya Mei 25 na sasa utachezwa Ijumaa ya Mei 23, huku wapinzani wao Chelsea wao watasafiri kuifuata Nottingham Forest katika mechi ya kuwania kufuzu UCL 2025-2026

Ikumbukwe Mei 25 itakuwa siku ya mwisho ya michezo ya ligi kuu ya Uingereza ambapo kwa kanuni za ligi hiyo mchezo yote ya mzunguko wa 38 inatakiwa kuchezwa siku moja ndani ya muda mmoja 

Kocha huyo raia wa Argentine pia amethibisha kuwa kipa wao Filip Jorgensen ataanza katika mchezo wa fainali wakati huohuo Christopher Nkunku na Marc Guiu bado wana hatihati ya kuukosa mchezo ho kutokana na majeraha yanayo wakabili.