( Aleksander Ceferin Rais wa shirikisho la soka barani ulaya UEFA)
Moja ya agenda kuu za mkutano huo ni kuhamisha mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya kutoka katika mji wa St. Petersburg wa nchini Urusi uliopanga kuchezwa tarehe 28 mwezi mei mwaka huu, wakihofia athari ya hali hiyo na maamuzi hayo kutangazwa leo ijumaa.
Upande mwingine mashirikisho ya soka ya nchi za Sweden, Poland na Jamhuri ya czech zimetoa taarifa ya pamoja wakisema hawataki kucheza mechi za mtoano za kufuzu kombe la dunia zilizopangwa kuchezwa mwezi ujao nchini urusi, wakihofia usalama wa timu zao. Russia wamepangwa kucheza dhid ya poland tarehe 24 mwezi march katika uwanja wa Dynamo Central mjini Moscow na mshindi wa mchezo huo atacheza na mshindi kati ya Sweden na Jamuhuri ya Czech mchezo uliopangwa kuchezwa aitha Urusi ama Poland.
(Uwanja wa Krestovsky uliopangwa kuchezwa fainali ya UEFA, Saint Petersburg nchini Urusi)
Kufuatia machafuko hayo klabu ya Manchester United imesema kuwa inafikiria kuvunja mkataba na kampuni ya ndege ya Urusi ya Aeroflot kutokana na sababu za vurugu hizo za kivita zinazoendelea kati ya Urusi na Ukraine. Na baada ya mmilikiwa klabu ya chelsea Roman Abramovic kuziliwa kuishi na hata kuingia nchini England kwa madai kumuunga mkono Rais wa UrusiVladimir Putin huku wadau wakihoji kama Abramovic atazuiwa na umiliki wake kwa klabu ya Chelsea.
Vile vile Klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani imetangaza kuondoa logo ya kampuni ya Urusi GAZPROM kwenye jezi yao ambayo ndio mdhamini mkuu wa klabu hiyo. Gazprom ni kampuni ya nchini Russia inayojihusisha na usambazaji wa gesi, lakini pia uwanja wa klabu hiyo wametangaza kuubbadilisha jina hivyo hautaitwa tena GAZPROM Stadium, maamuzi haya yote yamefikiwa baada ya Urusi kuanzisha vita kwa kuivamia Ukraine.


