Ijumaa , 13th Mei , 2016

Mshambuliaji Farid Mussa Malick anatarajia kuwasili nchini siku yoyote kuanzia leo hii akitokea nchini Hispania alipokuwa akifanya majaribio katika klabu ya Tenerife ya nchini humo.

Klabu hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza nchini humo ambayo inajulikana kama Segunda Division ikiwa ni hatua moja baada ya Ligi Kuu ambayo ni La Liga imekubali kiwango cha uchezaji cha winga huyo ambapo inasubiri kufanya mazungumzo na klabu yake ya Azam FC ili kuweza kumtwaa.

Farid alifanya majaribio nchini humo kwa takribani wiki mbili na ameonekana kukubalika na klabu hiyo.

Taarifa za ndani zinaeleza Tenerife na Azam FC wamekubaliana katika umiliki wa kinda huyo mwenye kasi ambaye imeelezwa anarejea nchini leo akitokea Hispania.