Jumamosi , 4th Aug , 2018

Timu ya Kikapu ya Flying Dribblers imekuwa timu ya kwanza kutinga fainali ya michuano ya Sprite Bball Kings baada ya kushinda kwa pointi 69 dhidi ya 63 za Team Kiza kwenye game 2 ya nusu fainali.

Mchezo kati ya Flying Dribblers (nyeusi) na Team Kiza (nyeupe).

Flying Dribblers ambao waliishia hatua ya nusu fainali kwenye michuano hii mwaka uliopita, wameshinda mechi mbili kwenye 'best of three' za nusu fainali hivyo kukata tiketi ya fainali moja kwa moja.

Kwenye game 1 Flying Dribblers walishinda pointi 84 kwa 75 za Team Kiza. Katika mechi ya leo nyota wa Flying Dribblers Baraka Mopele amefunga pointi 21 rebound 3 na Assist 1 hivyo kuipa tiketi ya fainali timu yake.

Kwa upande wa Team Kiza mchezaji Abdul Chingwengwe amefunga pointi 23, rebound 5 na Assist 2. Flying Dribblers sasa wanasubiri mshindi wa game 3 kati ya Portland dhidi ya Mchenga Bball Stars ili kujua wanakwenda kuchuana na nani kwenye fainali.

Michuano hii inayoandaliwa East Africa Television LTD na kudhaminiwa na kinywaji cha Sprite inampa nafasi bingwa ya kuibuka na kitita cha shilingi milioni 10, milioni 3 kwa mshindi wa pili na milioni 2 kwa mchezaji bora (MVP).