Jumatatu , 15th Mar , 2021

Timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars inashuka dimbani leo saa 9:00 Alasiri kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Kenya Harambee stars, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kueleka michezo ya kufuzu fainali za AFCON 2021.

Wachezaji wa Taifa stars

Taifa stars itacheza michezo miwili ya kirafiki na Harambee stars, ambapo mchezo wa kwanza unachezwa leo Machi 15, na mwingine utachezwa Machi 18, 2021.

Kocha wa Taifa stars Kim Poulsen atatumia michezo hii kama sehemu ya kukiandaa kikosi chake amabacho kitacheza michezo miwili ya kundi J' ya kuwania tiketi ya kufuzu michano ya AFCON.

Mchezo unaofata wa kundi J' Tanzania inacheza ugenini dhidi ya Equatoria Guinea, mchezo utakao chezwa machi 25, na mchezo mwingine utakuwa dhidi ya Libya ambao utapigwa jijini Dar es salaam hii ni michezo ya mwisho ya kundi hilo na Tanznaia ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 4 sawa na Equatoria Guinea walio nafasi ya pili, Tunisia ndio vinara wakiwa na alama 10 wakati Libya wanaburuza mkia wakiwa na alama 3.

 

Mchezo wa leo unachezwa katika Dimba la Nyayo.