
Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, kulikuwa na hofu kuwa kutokuwepo kwa Migi aliyejiunga na Azam FC, kungeweza kuidhoofisha APR katika Kombe la Kagame.
APR ilijitahidi kuomba kumtumia Migi katika michuano hiyo lakini mambo yalishindikana na sasa anaichezea Azam.
Timu hiyo ya Rwanda imetinga robo fainali baada ya kushinda mechi tatu mfululizo katika Kundi B na kujikusanyia pointi tisa ikifuatiwa na A Ahly Shandy yenye pointi nne.