Ijumaa , 24th Feb , 2017

Wanariadha watatu wa Urusi, wamesafishwa kurejea kwenye mashindano ya dunia na bodi ya mapitio ya Chama cha Riadha Duniani  IAAF.

Mwanamichezo Anzhelika Sidorova kutoka Urusi

Wanariadha hao, ni Anzhelika Sidorova, Kristina Sivkova na Aleksei Sokirskii, ambao watabaki kama washiriki binafsi, lakini ushiriki wao hadi uthibitishwe na waandaaji wa mashindano husika.

Watatu hao, wanaweza kushindana kwenye mashindano ya ndani ya Ulaya,  (European Indoor Championships) mjini Belgrade na mashindano ya kurusha vitu, (European Throwing Cup) mwezi ujao.

Shirikisho la Riadha Urusi, litaendelea kutumikia adhabu ya kutoshiriki mashindano ya kimataifa, baada ya kuhusishwa na kudhamini matumizi ya dawa za kuongeza nguvu kwa wanariadha wake.