
Indiana Pacers
Kwenye michezo yao mitano Indiana pacers wameshinda michezo minne ambapo kwa sasa wanasubiri mshindi kati ya Boston Celtics na New York Knicks ambao watashuka dimbani usiku wa leo Mei 14 2025
Mchezaji bora wa mchezo huo ni Tyrese Haliburton amefunga points 31 ,Rebound 6,Assist 8
Mchezo mwingine uliopigwa usiku wa jana ni Oklahoma City Thunder wameitandika Denver Nuggets vikapu 112-105 huku Shai Gilgeous-Alexander akifunga pointi 31 zilizowapeleka mbele kwa mabao 3-2 katika mfululizo wao wa nusu fainali ya kanda ya Magharibi.
Huku nyota wa Nuggets Nikola Jokic alifunga points 44 na rebounds 15, lakini hakuweza kuwazuia Oklahoma City kuibuka washindi katika mchezo wao wa tano wa playoff.