Ijumaa , 29th Oct , 2021

Mabingwa watetezi wa Serie A, Inter Milan imefanikiwa kumuongezea kandarasi ya miaka 4 mshambuliaji wake Lautaro Martinez hadi mwishoni mwa msimu wa mwaka 2025-2026.

(Mshambuliaji wa Inter Milan, Lautarao Martinez.)

Kumuongezea mkataba mshambuliaji huyo nyota, kumezima fununu za nyota huyo kuwekwa sokoni na kuhamia Barcelona kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari 2022.

Mkataba huo unamfanya Martinez awe mchezaji pekee anayelipwa zaidi kwenye kikosi hicho kwasasa lakini kutoweka kipengele cha kumzuia mchezajihuyo kuondoka endapo klabu yeyote ikimhitaji ‘Release Clause’.

Martinez alijiunga na Inter Milan mwaka 2018 akitokea klabu ya Racing ya nchini kwao Argentina, na tayari ameshacheza michezo 114, kufunga mabao 54 na kutoka assist 15 pamoja na kushinda ubingwa wa Serie A msimu wa 2020-21.