Alhamisi , 23rd Sep , 2021

Mchezaji wa kikapu wa Golden States Warriors, Andrew wiggins huenda akakosa ufunguzi wa michezo kuelekea msimu mpya wa NBA, baada kukataa kuchanja chanjo ya UVIKO-19. 

Nyota wa Golden State Warriors, Andrew Wiggins akijaribu kumtoka Nyota wa Lakers, Anthony Davis kwenye NBA msimu uliomalizika.

Wasi wasi huo umeibuka kutokana na sheria itakayoanza Oktoba 13, 2021 Jijini San Francisco, inapotokea Warriors, ambapo itaruhusu watu waliopata chanja ya UVIKO-19 pekee kuhudhuria mikusanyanyiko ya aina yoyote ikiwemo ya kimichezo pamoja na mazoezi.

Ikiwa hatapata chanjo, hataruhusiwa kushiriki katika michezo ya nyumbani ya Warriors. ambapo itakuwa hasara kwa Golden States na Wiggins mwenye wastani wa points 18.6 na ribaundi 4.9 wakati akifunga vikapu kwa wastani wa zaidi ya 47.7% na kutoka kwenye kina cha uwanja akifunga kwa asilimia 38%.

NBA iliziarifu timu mapema mwezi huu kwamba watalazimika kufuata sheria za chanjo za ndani ya mji yao. Ambapo mpaka sasa Miji miwili tu iliyopitisha sheria hiyo ni San Francisco na New York City.