Ijumaa , 22nd Oct , 2021

Kocha wa AS Roma, Mreno Jose Mourinho amekutana na kipigo Cha mabao 6-1 dhidi ya Bodo/Glimt ya Norway kwenye Mchezo wa UEFA conference league usiku wa Oktoba 21, ikiwa Ni kichapo Kikubwa yangu aache kufundisha Soka.

(Kocha wa AS Roma, Jose Mourinho akionekana kwenye matukio tofauti tofauti.)

Kipigo hiki ni sawa na kile Cha mabao 5-0 alichopokea kutoka kwa FC Barcelona katika Mchezo wake wa kwanza wa El Classico Mnamo mwaka 2010 akiwa Kocha wa real madrid.

Baada ya kichapo hicho, Kocha huyo maarufu Kama "The Special one" alisema kuwa yeye Ndo anastahili Lawama zote za Mchezo na matokeo hayo kutokana na maamuzi ya wachezaji Kucheza na aina ya mfumo ulikuwa Ni mpango kazi wake ambao haukufanya Kazi.

"Niliamua kucheza na safu hii, kwa hivyo jukumu ni langu," aliiambia Sky Sport Italia.

"Nilifanya hivyo kwa nia nzuri, kutoa nafasi kwa wale wanaofanya kazi kwa bidii na kubadilisha kikosi kwenye uwanja wa sintetiki katika hali ya hewa ya baridi".

"Sikuwahi kuficha ukweli kwamba tulikuwa kikosi chenye mapungufu ya kweli. Tuna wachezaji 13 ambao wanawakilisha timu moja, wengine wako kwenye kiwango tofauti."

"Tulipoteza dhidi ya timu ambayo ilionyesha ubora zaidi usiku wa leo." Alisema Mourinho.