
Kikosi cha Azam FC
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka TFF Alfred Lucas amesema, katika mechi namba 156 iliyozikutanisha Mbeya City dhidi ya Azam Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, katika benchi la ufundi la Azam FC kulikuwa na mapungufu yaliyopelekea kumchezesha Nyoni kinyume na sheria.
Lucas amesema, kwa mujibu wa kanuni ya 37 Azam fC imepoteza mchezo huo na imepokwa ushindi wa mabao matatu na kwa kutumia kanuni ya 14 ya Ligi Kuu toleo la mwaka jana Mbeya City imepewa ushindi huo.
Lucas amesema, benchi la ufundi katika kila timu linatakiwa kuwa makini ili kuweza kuweka kumbukumbu sawa za wachezaji wao kabla ya kuingia Uwanjani kwani bila kuwa makini kanuni zitakuwa zikiwagharimu kila mara.