Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kagera Sugar yakosa tamko juu ya usajili wake

Jumatano , 11th Jul , 2018

Baada ya tetesi kueleza kuwa klabu ya soka ya Kagera Sugar, imewasajili wachezaji watano kutoka klabu ya Ndanda FC ya Mtwara, timu hiyo ya mkoani Kagera imeshindwa kuthibitisha taarifa hizo.

Kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime

Akiongea na www.eatv.tv kocha mkuu wa Kagera Sugar Meck Mexime, amesema hajui lolote kuhusu usajili huo kwani hayupo na timu muda mrefu kwahiyo yote yanawezekana huenda wamesajiliwa au hawajasajiliwa.

''Mimi sijui kuhusu huo usajili, nachoweza kusema timu inafanya usajili lakini kwa hawa wachezaji watano kutoka Ndanda FC sina taarifa nao maana sikuwepo kwenye timu muda mrefu'', - amesema.

Tetesi zilizosambaa mitandao ni kuhusu wachezaji Jeremiah Kasubi ambaye ni mlinda mlango, walinzi Hemed Khoja, Ahmad Waziri, kiungo Majid Khamis na mshambuliaji Omary Mponda wote wakidaiwa kuikacha Ndanda FC na kusaini Kagera.

Kagera Sugar ambayo ilikuwa ikifanya vizuri katika misimu ya nyuma kwenye ligi kuu Tanzania Bara kiasi cha kumaliza kwenye nafasi 4 za juu, msimu uliopita haikuwa na msimu mzuri baada ya kumaliza katika nafasi ya 9 ikishinda mechi 8 kati ya 30 na kupoteza 9 pamoja na sare 13.

Jitihada za kuwatafuta viongozi wa Ndanda FC kulizungmzia hilo zimekwama baada ya kushindwa kupokea simu zao kila walipotafutwa.
 

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi