
Benchi la ufundi la Yanga.
Akizungumza na EATV kocha Kaze amesema mchezo ulikuwa mgumu licha ya kutengeneza nafasi nyingi lakini hawakucheza vizuri kama kawaida yao.
''Hatuwezi kutafuta visingizo hii ni timu kubwa , lakini naamini mchezo wetu ujao dhidi Tanzania Prison tutajituma na kadri ya uwezo wetu tupate alama tatu'' amesema Cedrick Kaze kocha msaidizi Yanga.
Katika msimamo wa ligi kuu Yanga imefikisha alama 56 baada ya mechi 21 na kuiacha Simba kwa tofauti ya pointi 13 huku Ruvu Shooting wakibakia nafasi 14 wakiwa na pointi 22.