Jumatatu , 19th Apr , 2021

Vilabu 12 barani Ulaya vimekubaliana na kutangaza mashindano yao mapya yanayoitwa European Super League.

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez anatajwa kuwa na nguvu katika kukamilika kwa mchakato wa uanzishwaji wa mashindano mapya Ulaya.

Vilabu hivyo ni AC Milan , Inter Milan, Juventus , Barcelona , Real Madrid, Atletico Madrid, Chelsea, Manchester City, Manchester United, Liverpool, Arsenal na Tottenham wote wamejiunga kwenye hiyo ligi.

Vilabu 3 zaidi vinatarajiwa kujiunga kuwa kama katika orodha ya vilabu anzilishi kabla ya kuanza kwa msimu wa kuzindua, ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kaunza mapema iwezekanavyo.

MUUNDO WA SUPER LEAGUE

1:Mwenyekiti-FlorentinoPerez ( Real Madrid )

2:M/ Mwkt- Andrea Agnelli ( Juventus )

3:M/ Mwkt - Joel Glazer ( Man United )

UEFA, FIFA na vyama/ mashirikisho ya soka wametangaza watapingana vikali na uanzilishi wa ligi hiyo .

Taarifa ya UEFA ,” Kila klabu na kila mchezaji ambaye atashiriki mashindano ya Super League watafungiwa kushiriki mashindano ya ligi ya mabingwa Ulaya na mashindano ya kimataifa ya FIFA, mataifa Ulaya . “

Vilabu kutoka Uingereza vitahitaji ruhusa ya FA kushiriki mashindano hayo mapya na taarifa ya FA inasema kwamba hawatotoa ruhusa maana yake vilabu vya EPL vitahitaji kujitoa kwenye ligi ya Uingereza moja kwa moja ili kushiriki Super League .

MUUNDO WA ESL

Kutakuwa na timu 20 zikatazoshiriki mashindano hayo , 15 timu anzilishi na zingine 5 zitapatikana kwa kufuzu kutokana na mafanikio ya msimu husika kwenye mashindano ya ligi za nchi husika

Mechi za michuano hiyo zitakuwa zinachezwa katikati ya wiki ambapo wikiendi vilabu vitaendelea kushiriki katika ligi zao za nyumbani kama kawaida.

Mashindano yatakuwa yanaanza mwezi Agosti kutakuwa na makundi mawili ya timu 10. Watacheza nyumbani na ugenini, ambapo watatu wa juu katika kila kundi watafuzu moja kwa moja hatua ya robo fainali. Timu zilizomaliza nafasi ya 4 na 5 watacheza mtoano kwenye mechi mbili za nyumbani na ugenini kupata timu mbili zingine za kucheza robo fainali.

Robo na nusu fainali zitakuwa za nyumbani na ugenini na Fainali moja itakayochezwa uwanja “ Neutral “ . Mara tu ya kuanza kwa mashindano ya wanaume na mashindano ya wanawake yatafuata .

DHUMUNI KUBWA

Kuongeza mapato kwa vilabu na kukuza uchumi ambao itaendana na ukuaji wa soka la ulaya na malipo yatakuwa makubwa zaidi ya ambayo yanatokana na mashindano ya Ulaya ya sasa.
 

Vilabu anzilishi vitapokea kiasi cha Dola Bilioni 3 ili kuunga mipango yao ya uwekezaji katika miundombinu na kukabiliana na athari zilizoletwa na Covid-19 .