Mkataba wa Mbappe na PSG unamalizika mwisho mwa msimu huu wa 2021-22
"Kwa kweli, katika wiki moja mchezaji wa Real Madrid Karim Benzema, kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti na sasa Rais Florentino Perez wanazungumza juu ya Kylian kama tayari ni nchezajiwao. Ninarudia, huu ni ukosefu wa heshima ambao hatuwezi kuvumilia." Amesema Leonardo
Mbappe mwenye umri wa miaka 22 mkataba wake na PSG unamalizika mwishoni mwa msimu huu wa 2021-22, na siku mbili zilizopita mshambuliaji huyo aliweka wazi kuwa mwezi Julai aliuomba uongozi wa PSG umuuze ili wapate fedha itakayotumika kumsajili mchezaji mwingine ambaye ataziba nafasi yake lakini pia asiondoke bure, lakini uongozi haukumjibu.
Utata huu umejitokeza baada ya hapo jana Rais wa Los Blancos Forentino Perez kusema hivi karibuni kutakuwa na makubaliano ya Real Madrid kumsajili Mbappe
“Mwezi Januari tutakuwa na habari kuhusu Mbappe, tunatumahi kuwa mnamo Januari 1, 2022 kila kitu kitakuwawazi." Amenukuliwa Perez .
Mbappe alijiunga na PSG msimu wa 2017-18 akitokea AS Monaco, na ataondoka bure endapo kama PSG haitamuuza katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari au kama hatasaiini mkataba mpya.





