
Kiungo huyo amerejea kikosini wiki iliyopita baada ya kukaa nje tangu Novemba mwaka jana, alipokwenda kwao Rwanda katika majukumu ya timu ya taifa.
Pluijm asema kiungo huyo bado hajawa fiti kwa ajili ya kumtumia, badala yake anatakiwa kuongeza bidii mazoezini ili kurejesha kiwango chake kwani alikuwa nje muda mrefu.
Hans amesema, Haruna bado hajawa fiti na anatakiwa kujituma zaidi ili kuwa fiti na hata mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Friends alikuwa asicheze lakini alilazimika kucheza kwa kuwa Said Makapu alifiwa na kaka yake na mazishi yalikuwa siku hiyo.