Ijumaa , 22nd Jan , 2021

Klabu ya Simba SC itakuwa na mkutana na waandishi wa habari leo Ijumaa Januari 22, 2020. mkutano huu unaangaziwa na wadau wengi huenda klabu hiyo ikamtangaza kocha mpya atakae kinoa kikosi hicho, baada ya mabingwa hao wa Tanzania bara kuachana na Kocka Sven Vandenbroeck.

Kocha wa AS Vital na timu ya taifa ya DR Congo, Florent Ibenge ni moja ya kocha anaetajwa sana huenda akawa kocha mpya wa Simba SC

Kwa sasa kikosi hicho cha wekundu wa msimbazi kipo chini ya kocha msaidizi Selemani Matola, baada ya uongozi wa timu hiyo kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na aliyekuwa kocha wa kikosi hicho mbeligiji Sven Vandenbroeck ambae ametimkia AS FAR ya Morocco.

kwa mujibu wa taarifa mbalimbali makocha kadhaa wamekuwa wakihusishwa kujiunga na kikosi cha Simba ambacho kipo hatua ya makundi klabu bingwa Afrika msimu huu.

Kocha wa timu ya taifa ya Jamhuri ya kidmokrasia ya Kongo na klabu ya AS Vital Florent Ibenge amekuwa akihusishwa zaidi kwani kuna baadhi ya picha za kocha huyo ameonekana akiwa kwenye mazungumzo na mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

Lakini pia kocha wa zamani wa vilabu vya Yanga, Sports Club Villa, Al Hilal Oumdurman na Al Ahly ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Taifa ya Zambia Milutin Sredojević maarufu Micho nae anahusishwa.

Makocha wengine wanaotajwa ni pamoja na kocha raia wa ubeligiji Ivan Jacky Minnaert, Stephen Kean raia wa Scotland pamoja na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda Sébastien Desabre.

Simba ambao ni mabingwa wa Tanzankia bara kwa misimu 3 mfululizo wamepangwa kundi A, kwenye michuano ya ligi ya mabingwa sambamba na mabinngwa watetezi Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Congo DR na AL Merrick ya Sudani, na malengo ya timu hiyo ni kufika hatua ya nusu fainali kwenye michuano hii.

Na imekuwa inaripotiwa kuwa kocha anaetafutwa ni kocha mwenye uzoefu na kulijua soka la Afrika, ili aweze kutimiza malengo ya mabingwa hao wa Tanzania bara.