Jumatano , 29th Jan , 2020

Leo Januari 29, utapigwa mchezo wa ligi kati ya Simba na Namungo FC katika uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam.

Simba SC

Kuelekea mchezo huo, kocha wa Namungo FC, Hitimana Thiery amesema kuwa ataingia na mbinu mpya ambayo itawasaidia kuwafunga Simba na kuondoka na pointi tatu huku akiwapa heshima wapinzani wao kuwa ni mabingwa wa nchi na ni lazima wapewe tahadhari kubwa.

Mchezo wetu utakuwa mgumu na wenye ushindani, unapocheza na bingwa lazima uwe na tahadhari kabla hajakuumiza tunalitambua hilo na tutaingia uwanjani kwa tahadhari tukiwa na malengo ya kuzipata pointi tatu muhimu, mashabiki watupe sapoti", amesema Thiery.

Simba na Namungo FC zinakutana kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu Tanzania Bara huku Simba wakiwa ni vinara kwa pointi 41 katika michezo 16 iliyocheza mpaka sasa, Namungo FC ikiwa na pointi 28 katika nafasi ya tano baada ya kucheza mechi 15.