Kushoto ni Kaseja na kulia ni Manula
Akiongea kwenye Kipenga Xtra ya East Africa Radio Kaseja amesema mashabiki wanakosea kumlinganisha na Manula badala yake wanapomtaja wanatakiwa wawataje makipa wote wakiwemo Shaban Kado, Menata Mnacha na wengine.
"Hakuna ugomvi kati ya Juma na Manula, magolikipa wengi sana ni wadogo zangu na najua wanahitaji msaada kutoka kwangu, kwahiyo tusitengeneze ugomvi badala yake tushirikiane ili wawe bora kunizidi hata mimi'', amesema.
Kuhusu kuachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Heroes' ambacho kinakwenda kushiriki CECAFA Seniour Challenge Cup nchini Uganda, amesema ni kwasababu ya majeruhi na sio kutoelewana na Manula kama inavyoelezwa.
'Kuhusu mimi kuachwa kwenda CECAFA ni kweli siendi kwasababu naumwa goti na daktari kanishauri nipime kipimo cha MRI ili tujue maana nimekuwa nikiumwa muda mrefu' - Kaseja